Oct 6, 2013

Kiarabu ni Lugha Pekee Iliyo kamilika.

SHEIKH KILEMILE AKIWASILISHA MADA MBELE YA WANA SEMINA

Imeelezwa kwamba Lugha Pekee iliyo kamilika hapa duniani ni Lugha ya Kiarabu.

Maelezo hayo yamesemwa leo hii na Sheikh Suleiman Kilemile alipokuwa anawasilisha mada ya umuhimu wa kujifunza Lugha ya Kiarabu.

Alisema Lugha ya kiarabu ni Lugha pekee iliyotimia kwa kuwa na umoja,uwili na utatu tofauti na lugha nyengine.

Ndugu wana semina,ukamilifu wa Lugha ya Kiarabu unatokana na Mwenyezi Mungu kuiichagua Lugha ya kiarabu na akatia maneno yake (kwa maana ameiteremsha Qur aan kwa kutumia Lugha ya Kiarabu).

Naomba mufahamu kuteremshwa Qur aan kwa Lugha ya kiarabu kumeimarisha zaidi Lugha hiyo.

Aliwataka watu waachane na hisia kwamba Lugha ya kiarabu ni Lugha ya waarabu pekee au ni Lugha ya Waislam,bali waichukuwe Lugha ya Kiarabu Kuwa ni Lugha ya mawasiliano.

Alisema Kiarabu ndiyo Lugha pekee ambayo hata nchi zisizo za kiislamu kama Jordan wanaitumia kwa kasi ya juu baada ya kuona umuhimu wa Lugha hiyo katika mawasiliano.

Wakati huo huo Sheikh Kilemile aliwataka waislamu kuitumia Lugha ya Kiarabu ili Kurahisisha ufahamu wao katika kujifunza elimu ya Dini ya Kiislamu.

"Naomba niwapeni siri,njia nyepesi ya kufupisha masafa ya kusoma,ni kujifunza na kuitumia Lugha ya Kiarabu,nasema hivi kwa sababu,vitabu vyote vya kiislamu vimeandikwa kwa lugha ya kiarabu,sasa ikiwa hujuwi Lugha ya kiarabu itakuchukuwa muda mrefu kuvielewa",mwisho wa kumnukuu.

Akionekana kubobea katika Lugha ya Kiarabu Sheikh Kilemile amesema,kutokana na kutokuwa na utayari wa kujifunza Lugha hiyo,imepelekea watu wengi kuitumia kwa makosa.

Akitoa mfano kadhaa alisema,leo neno KAASUN linatafsiriwa kuwa ni GLASS,tafsiri hii siyo sahihi,bali Neno KAASUN litakuwa ni sahihi kulitafsir Glass pindi Glass hiyo ikiwa ina maji.

Akifafanua zaidi alisema,Glass ikiwa haina maji kwa Kiarabu inaitwa ZUJAAJATUN.

Semina hiyo ya siku tatu itakhitimishwa kesho Inshaa ALLAAH

SEHEMU YA WASHIRIKI WAKIFUATILIA SEMINA HIYO.


0 comments:

Post a Comment