Vyombo vya habari vya Misri vinaripoti kuwa serikali
ya nchi hiyo imemtia mbaroni mwanasiasa maarufu Essam El Arian ambaye
pia alikuwa ni mwanachama wa Muslim Brotherhood na Makamu Mwenyekiti wa
chama cha Justice and Freedom ambacho pia ni sehemu ya Muslim Brotherhood.
Kukamatwa kwa kiongozi huyo ni moja ya hatua ya serikali iliyopo madarakani kudhibiti hatakati zinazoendeshwa na kundi hilo lenye itikadi kali za kiislamu ambazo zimepigwa marufuku.
Shirika la habari la serikali la Misri, Mena, limesema Bwana Erian anatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo pamoja na Rais aliyoondolewa madarakani Mohammad Morsi na maafisa wengine wa Muslim Brotherhood.
Picha zilizosambazwa kwenye vyombo vya habari vya Misri zinaonyesha kitendo cha kukamatwa kwake ambapo Bwana Erian anaonekana akiwa na tabasamu amesimama karibu ni mifuko miwili.
0 comments:
Post a Comment