Waokozi nchini Niger wanasema kuwa wamepata miili 87
ya watu waliofariki baada ya magari yao kuharibika walipokuwa wanajaribu
kuvuka jangwa la Sahara.
Niger ni kivukio kikubwa cha wahamiaji wanaokuwa safarini kufika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuelekea Ulaya.
Lakini wengi wa wanaofanikiwa kukamilisha safari hiyo huishia kufanya kazi katika mataifa ya Afrika Kaskazini.
Kulingana na Bwana Alhacen, moja ya magari ambayo wahamiaji hao walikuwa wanatumia kwa usafiri, liliharibika walipotoka mji wa Arlit mwishoni mwa mwezi Septemba, au mwanzoni mwa Oktoba.
Maafisa wa usalama pia wamesema kuwa gari la pili liliharibika lilipokuwa njiani kurejea Arlit ili kutengenezwa.
Inaonekana kuwa miongomi mwa wasafiri hao takriban watu 10 walisafari kurejea Arlit na kutoa taarifa ya wenzao kukwama jangwani.
Iliarifiwa kuwa miili mitano ilipatikana.
Mnamo siku ya Jumatano, wafanyakazi wa kujitolea pamoja na wanajeshi, walipokuwa wanawatafuta wahamiaji hao, wakafanikiwa kupata maiti zaidi umbali wa kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Algeria.
Kati ya maiti 48 waliopatikana, kulikuwa na miiili ya watoto na vijana na Alhacen alisema kuwa walikuwa wanaelekea nchini Algeria kutafuta vibarua vya mishahara midogo sana.
0 comments:
Post a Comment