Oct 9, 2013

INNAA LILLAAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN

AL MAR HUUM SHEIKH MUHAMMAD SHARIF FAMAU


 SHEIKH ABDALLAH BAWAZIR,MTOA TAARIFA

Sheikh Muhammad Sharif Famau wa Mlindi Kenya amefariki Dunia.

Kwa mujibu wa Sheikh Abdallaah Bawazir,Sheikh Famau amefariki jana usiku na anatarajiwa kuzikwa leo.

Akitoa wasifu wa Mar huum,Sheikh Bawazir amesema Sheikh Famau alikuwa ni mwanachuoni mkubwa aliyesoma kwa Sheikh Harith bin Swaleh wa Lamu Kenya.

Katika chuo kikuu cha Madina mar hum Famau alisoma na masheikh mbalimbali wa hapa Tanzania.

Sheikh Bawazir aliwataja masheikh hao kuwa ni Sheikh Juma Pori,Sheikh Muharram Juma Doga,Sheikh Twaha Suleyman Bane,Sheikh Hamid na wengineo.

Munira blog inawapa pole wafiwa wote.
Allah amrehemu

1 comments: