Oct 3, 2013

Gari Laponda Kichwa Cha Mtoto.

Mwanafunzi mmoja amefariki baada ya kugongwa na gari.

Tukio hilo limetokea muda mfupi uliopita maeneo ya mbagala kizuwiani manispaa ya Temeke mkoa wa Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mpasha habari wetu amesema mtoto huyo ni mwanafunzi ambaye hakuweza kujulikana mara moja jina wala shule anayosoma,amekutwa na umauti huo wakati anavuka barabara katika Zebra.

Akiendelea kuipasha munira blog,bwana Al Walid Mabuga ambaye alifika eneo la tukio muda mfupi baada ya kutokea amesema "Nimemkuta mtoto akiwa bado hajaondolewa eneo la tukio,kwa hakika inasikitisha,kwani kichwa kimesagika kabisa,hauwezi kuitambua sura yake"mwisho wa kumnukuu.

Aliendelea kusema tukio hilo limesababisha Taharuki kiasi Jeshi la polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliochukizwa na tukio hilo..

Inasemekana dereva wa gari lililosababisha ajali alijaribu kukumbia lakini boda boda zilimfukuza na kumkamata na anashikiliwa na jeshi la polisi.

Munira Blog inaendelea na juhudi za kumtafuta kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke Kuzungumzia tukio Hilo.

0 comments:

Post a Comment