MWENYEKITI WA IDARA YA MADRASA DYCCC SHEIKH OMAR AWADH AKIZUNGUMZA NA WALIMU WA MADRASA WAKATI WA SEMINA HIYO ILIYOFANYIKA LEO HII.
Walimu wa Madrasa nchini wametakiwa kuboresha Madrasa zao ili kuzifanya ni za kisasa zenye kwenda sambamba na dunia ya sasa.
Hayo yamesemwa leo hii na Mwenyekiti wa Idara ya Madrasa DYCCC sheikh Omar Awadh alipokuwa anafungua semina ya utafiti wa misikiti nchini Tanzania.
Amesema licha ya kuwapongeza kwa kazi mzuri na ngumu ya kufundisha watoto wetu,lakini kuna ulazima wa kubadilika kwa makusudi kutoka katika hali iliyozoeleka na kwenda katika mazingira ya kisasa.
"Tukiwa ni walimu wa madrasa heshima yetu itazidi kama tutaboresha madrasa zetu kwa kuzifanya ni za kisasa zaidi,ifikie hatua madrasa zetu ziwe na mfumo wa utawala bora,uongozi imara wenye kujumuisha wazazi lakini pia tuwe na ofisi,leo kuna madrasa zimepiga hatua kubwa,zina mitandao,zina vipeperushi na harakati mbalimbali za kimaendeleo,ndugu zangu waalimu tujitahidi kufikia hatua hiyo".
Awali aliwataka walimu kuwa waitumie vizuri SACCOS ya walimu wa idara hiyo ambayo itaanza kutoa mikopo mwezi wa kumi mwaka huu.
Sambamba na hilo aliwataka walimu kuwa na mtandao utakao wawezesha kuchunga taratibu za pamoja katika kuhama na kuhamia wanafunzi kutoka madrasa moja.
Aidha aliahidi idara yake kuwadhamini walimu wengine katika madrasa ambazo zinawanafunzi wengi.
kwa sasa idara ya madrasa DYCCC inawadhamini walimu wa madrasa 48.
KUTOKA KUSHOTO NI SHEIKH OMAR AWADH,SHEIKH ABDALLAAH BAWAZIR,SHEIKH YASIR SALIM NA SHEIKH YUSUF KUNDECHA WAKIWA KATIKA SEMINA YA WALIMU WA MADRASA SAMBAMBA NA UZINDUZI WA SEMINA YA UTAFITI WA HALI HALISI YA MISIKITI NCHINI TANZANIA ILIYOANDALIWA NA HAY ATUL ULAMAA.
SEHEMU YA WAALIMU WA MADRASA WAKIWA KATIKA SEMINA