Oct 23, 2013

BUSARA ZA KIKWETE ZIMEFUFUA MATUMAINI



MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMESEMA KUWA BUSARA ZA RAIS WA TANZANIA, JAKAYA KIKWETE ZIMEFUFUA MATUMAINI YA WANANCHI WENGI KUWEZA KUPATIKANA KATIBA MPYA, BAADA YA KUJITOKEZA CHANGAMOTO AMBAZO ZILIWAFANYA KUANZA KUVUNJIKA MOYO. 

MAALIM SEIF AMEYASEMA HAYO KATIKA HOTELI YA SERENA MJINI DAR ES SALAAM ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA BALOZI WA IRELAND NCHINI TANZANIA, FIONNUALA GILSENAN KUHUSU MAMBO MBALI MBALI, IKIWEMO MAENDELEO YA MCHAKATO WA KUPATIKANA KATIBA MPYA TANZANIA.

AMESEMA KUWA BAADA YA KUJITOKEZA MALALAMIKO YALIYOTOKANA NA KULETWA MSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, RAIS KIKWETE OKTOBA 14 MWAKA HUU ALIAMUA KUKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYOTE VYA SIASA NCHINI.

AMESEMA KATIKA MAZUNGUMZO YA RAIS NA VIONGOZI WA VYAMA VYOTE VYA SIASA NCHINI, WALIKUBALIANA VIONGOZI WA VYAMA HIVYO WAWASILISHE MAPENDEKEZO YAO YATAKAYOSAIDIA KUPATIKANA KATIBA NZURI NA KUMALIZA MALALAMIKO NA MIVUTANO ILIYOJITOKEZA.

MAALIM SEIF AMESEMA KUWA PANDE HIZO ZILIKUBALIANA KWAMBA MAZUNGUMZO HAYO YATAENDELEA NA YATAKUWA CHINI YA KITUO CHA DEMOKRASIA NCHINI (TCD), AMBAPO VYAMA VYOTE VYA SIASA VITAKUWA NA FURSA YA KUTOA NA KUWASILISHA YALE WANAYOONA YANAPASWA KUWEMO NA KUTOLEWA ILI BAADAYE YAFIKISHWE BUNGENI KWA AJILI YA KUCHUKULIWA HATUA.

AMEELEZA KUWA BAADA YA HATUA HIYO YA RAIS KIKWETE KUKAA PAMOJA NA WADAU MUHIMU KATIKA ZOEZI LA KUTAFUTA KATIBA MPYA, VIONGOZI WA VYAMA WAMEFURAHI NA WAKO TAYARI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUFANIKISHA LENGO LILILOKUSUDIWA.

AIDHA, BALOZI HUYO WA IRELAND AKIZUNGUMZIA HAJA YA KUDUMISHWA AMANI NA UTULIVU, ALIKUBALIANA NA USHAURI WA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, JUU YA HAJA YA MATAIFA KUSHIRIKIANA KATIKA KUPIGA VITA MATUKIO YA UVUNJIFU WA AMANI PAMOJA NA UGAIDI.

BALOZI GISLENAN AMESEMA KUWA VITENDO VYA UGAIDI HAVINA MIPAKA NA NCHI YOYOTE ILE INAWEZA IKALENGWA, KAMA ILIVYOJITOKEZA HIVI KARIBUNI NCHINI KENYA.

0 comments:

Post a Comment