Oct 23, 2013

Wakulima wanatudai Bilioni 17-KIKWETE



Rais Jakaya Kikwete, amesema ni aibu Serikali kudaiwa na wakulima wa Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe ambao wameiuzia mahindi yao. Kutokana na hali hiyo , aliwahakikishia wakulima hao kulipwa fedha zao haraka iwezekanavyo.


Rais Kikwete aliyasema hayo juzi kwa nyakati tofauti wilayani humo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kukagua, kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.“Ni kweli Serikali inadaiwa sh. bilioni 17 ambazo ni deni la wakulima wa mikoa mbalimbali nchini ambao walituuzia mahindi yao msimu uliopita kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),” alisema. 
 
Akipokea Ripoti ya Maendeleo wilayani humo, Rais Kikwete alisema wakulima wa Wilaya hiyo pekee bado wanaidai serikali sh. bilioni 3.115 za mahindi tani 6,231 waliyoyauza NFRA.Alisema hadi sasa wakulima wilayani humo wamelipwa shilingi bilioni 2,839 zilizotokana na tani 5,679 za mahindi ambapo NFRA ililenga kununua tani 13,000 lakini imeweza kununua tani 11,911 ingawa sehemu kubwa ya kiasi hicho hakijalipiwa na Serikali. 
 
 “Hii ni aibu, Serikali haiwezi kudaiwa na wakulima hivyo hizi fedha zitalipwa tu,” alisema Rais Kikwete na kuelezea hatua binafsi alizochukua kuhakikisha deni hilo linalipwa.Aliongeza kuwa, Serikali itaangalia uwezekano wa kununua tani 2,972 za mahindi ya msimu uliopita zilizobakia mikononi mwa wakulima wa Wilaya hiyo. 
 
 “Nimeambiwa NFRA bado inahitaji tani 40,000, ili kukamilisha shehena ya idadi ya tani 250,000 za mahindi kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa mwaka huu...nitawaambia waangalie kama kuna uwezekano wa kununua tani zilizobaki kwa wakulima wa Ludewa,” alisema. 

  Rais Kikwete pia alizungumzia maombi ya wananchi wa Ludewa kutaka Serikali inunue meli ili kuchukua nafasi ya Mv. Mbeya iliyozama katika Ziwa Nyasa ili kurahisisha usafiri ndani ya ziwa hilo ambalo linapakana na Wilaya hiyo. 

  Alisema Serikali itanunua meli kwa kwa ajili ya usafiri katika Maziwa Makuu nchini, kabla ya mwaka 2015 na zinaweza kuwa mbili badala ya moja katika Ziwa Nyasa, Victoria, Tanganyika. 

“Tunajua kuwa meli ya Mv. Mbeya ilizama katika Ziwa Malawi na nyingine katika maziwa mengine makubwa ya Tanganyika na Victoria...mimi katika kampeni zangu niliahidi nitanunua meli moja kwa kila ziwa,” amesema Rais Kikwete na kuongeza; 

 “Tumeagiza meli tatu kutoka Korea Kusini kwa sasa zinajengwa, pia tumeagiza meli nyingine tatu kutoka nchini Denmark nazo zinajengwa hivyo tunaweza kupata meli zaidi ya moja katika maziwa yote matatu na mbili nitazizindua kabla ya kumaliza kipindi changu cha uongozi mwaka 2015,” alisema. 

  Al isema kero nyingine zilizoibuliwa na wakazi wa Wilaya hiyo pamoja na ujenzi wa daraja kwenye Mto Ruhuhu, litajengwa. 

  Wakati huo huo, Rais Kikwete amewaonya wananchi wa Wilaya hiyo wasiwe hodari wa kuuza ardhi na mashamba yao ambayo yatakuwa na umuhimu mkubwa miaka michache ijayo kutokana na matunda makubwa ya uwekezaji. 

  Alisema Serikali inatarajia kuwekeza katika miradi ya chuma, makaa ya mawe na madini mengi yanayopatikana wilayani humo..Rais Kikwete aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo na kusisitiza kuwa; Msipochangamka mapema na kuanza kuangalia namna ya kunufaika na rasilimali za hapa, mtageuka ‘manokoa’ wa watu wengine kwenye ardhi yenu wenyewe,” alisema Rais Kikwete a, wakulima wilayani humo wamelipwa sh. bilioni 2.839 zilizotokana na tani

0 comments:

Post a Comment