Sep 10, 2013

WATAALAMU KUCHUNGUZA MSIKITI

Jopo la watalaamu wa Wilaya ya Dodoma, litachunguza mabaki ya udongo wa jengo la Msikiti wa Manyema, uliongua mwishoni mwa wiki ili kujiridhisha na hali ya usalama wa vyumba vilivyonusurika na kujua kama vinafaa kwa matumizi.
 
Hayo yalisemwa jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma, Stephen Humba, alipokuwa akizungumza na gazeti hili, kuhusu tukio hilo.
Wanaounda jopo hilo ambalo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi, mhandisi wa wilaya, Kikosi cha Zimamoto, polisi, ofisa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Idara ya Afya.
Humba alisema jopo hilo lilitembelea eneo la tukio Ijumaa iliyopita na kugundua kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.
“Walikubalina kuwa wachukue mabaki ya udongo katika jeno hilo kwa ajili ya kwenda kuupima katika maabara ili kuona kama jengo hilo litafaa kukarabatiwa ama la,”alisema.
Moto huo ulitokea Ijumaa iliyopita na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na jengo hilo.
Dk. Nchimbi alimuagiza Humba kuunda jopo la wataalam ili kuchunguza kama vyumba vilivyobaki vinaweza kutumiwa na waumini ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa binadamu.

0 comments:

Post a Comment