PACHA Kudra Hamad aliyebaki hai baada ya kufanyiwa upasuaji wa
kuwatenganisha na mwenzake, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa njia ya
haja kubwa.
Mama wa mtoto huyo, Pili Hija (24), aliliambia gazeti hili jijini Dar
es Salaam jana kuwa madaktari wamemuambia mtoto huyo atafanyiwa
upasuaji Alhamis wiki hii.
“Mwanangu anaendelea vizuri kwa sasa, nimeambiwa na madaktari kuwa
watamfanyia upasuaji sehemu ya haja kubwa Alhamis,” alisema Hija.
Mtoto huyo aliokolewa na jopo la madaktari bingwa saba wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa
(Moi) katika upasuaji uliofanyika mwezi uliopita. Mtoto huyo alizaliwa
bila kuwa na sehemu ya haja kubwa.
Hata hivyo, Ofisa Uhusiano wa Moi, Almas Jumaa alipopigiwa simu ili
kuthibitisha kama mtoto huyo atafanyiwa upasuaji siku hiyo simu yake
ilikuwa inaita bila kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment