Sep 12, 2013

Wahamiahaji Wadai Kunyanyaswa.

Inadaiwa oparesheni ya kimbunga inayoendeshwa na Serikali ya Tanzania yenye nia ya kuwaandosha wahamiaji haramu imeingia dosari baada ya baadhi ya wahamiaji kudai wana nyanyaswa na maofisa wa uhamiaji katika mikoa mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na munira blog baada ya kufanya mahojiano na baadhi ya wahamiaji hao katika mkoa wa Kigoma.

"Hili suala la sisi kurudishwa makwetu kwa njia ya amani mimi sijaona mbaya lakni tatizo mifugo yangu na baadhi ya mali zangu nimenyang'nywa na maofisa wa uhamiaji kitu ambacho kinazidi kutuweka katika hali ngumu" alisema Bwana kavumba akiwa mpakani mkoani kigoma.

Blog hii ilishuhudia baadhi ya watu wakipinga kuondoka kwa madai kwamba wao si wahamiaji h
aramu bali ni Watanzania halisi.
"ona mwandishi wa habari,hiki hapa ni cheti changu cha kuzaliwa,lakin pia hizi ni kadi za klinik za watoto wangu,nasaba (ukoo) yangu yote ipo hapa hapa Tanzania,leo wananiambia mimi si mtanzania,wananipeleka wapi na nitaishi vipi huko",alisema baba wa familia moja pasipo kutaja jina lake.

Wakati Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe Jakaya Kikwete akizindua oparesheni hiyo alisema itafanywa kwa uangalifu mkubwa pasipo kukiuka haki za kibinaadamu.

Hivi karibuni kuna taarifa ya mtu mmoja kujinyonga ikiwa ni kupinga kurejeshwa kwao baada ya kudai kwamba ameishi hapa nchini tangu miaka ya sabini.

0 comments:

Post a Comment