Sep 14, 2013

TUNALAANI- CUF


Chama cha wananchi CUF kimelaani vikali kitendo cha kumwagiwa tindi kali kwa Padri wa kanisa katoliki Cheju Zanziba Anselmno Mwangamba jana jioni katika maeneo ya Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Akizungumza na mwandishi wa habri hizi Mkurugenzi wa haki za binadamu habari uenezi na mawasiliano ya Umma Mh,Salim Bimani amesema kuwa matendo ya kihalifu yanazidi kuongezeka siku hadi siku ndani ya Zanzibar bila ya wahusika kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Amesema tukio hili la kumwagiwa tindi kali kwa Padri si la kwanza wala la pili huku jeshi la Polisi likiwa bado halijawashika wahusika wa matukio haya ambao kwa makusudi wamekuwa na nia ya kuichafua Zanzibar kimataifa.

Ameitaka Serikali SMZ kupitia Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa wanafanya kila jitihada za kuwakamata wahusika na hatimae kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkono wake na hatimae kukomesha kabisa vItendo hivi vya kihalifu ndani ya Zanzibar.

Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili waweze kuwashikilia waliohusika na tukio na sio kukamatwa wasiohusika jambo ambapo linaipelekea jamii kujenga picha mbaya na jeshi hilo.

Aidha Mh,Bimani ametoa wito kwa wazanzibar wote wanaoipenda nchi yao kutoa ushirikiano wa kina kwa jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wa matukio haya ya kihalifu.

0 comments:

Post a Comment