Sep 16, 2013

Polisi chimbueni mzizi wa Tindikali-Sheikh Mtata


Umoja wa Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania kupitia Katibu Mkuu wake, Hamis Mataka amelitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kuwajibika ipasavyo na kuwapata watu waliohusika na unyama huo dhidi ya Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Zanzibar, Anselmo Mwang’amba

Sheikh Mataka alisema kama matendo ya kinyama ya watu kumwagiwa tindikali hayatafanyiwa kazi na mzizi wa uasi huo kuchimbuliwa amani ya nchi itatoweka.

“Lazima Jeshi la Polisi lifanye kazi yake kwani hali si nzuri na kutokana na matukio hayo kufululiza. Kimsingi matukio haya yanaweza kuzua hisia mbaya za udini na uzanzibar na ubara, hivyo yakomeshwe mara moja,” alisema Sheikh Mataka.

Alisema vyombo vya dola vinapaswa kutimiza majukumu yake ya kulinda amani na mali za watu vinginevyo historia ya Zanzibar kwamba ni eneo tulivu lenye amani itatoweka na kuonekana kuwa ni eneo lisilofaa kuishi kwa watu ambao si wazawa wa eneo hilo.

Shekh Mataka alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Padre Mwang’amba na kwamba yeye kama kiongozi wa dini hataacha kuonya na kuelekeza kisha kuwaachia wahusika kutenda sawasawa na nafasi zao zinavyowataka kuwajibika.

 RAIS WA SERILKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MHE DK MUHAMMED SHEIN AKIMJULIA HALI PADRI MWANG'AMBA.

0 comments:

Post a Comment