Hili ni Jengo lililoshambuliwa la chama cha udugu wa Kiislamu mjini Cairo.
Serikali ya Misri imeyafunga makao makuu ya gazeti "Uhuru na Haki"
ambalo linalomilikiwa na chama cha Udugu wa Kiislamu ikiwa ni hatua ya
mwanzo yenye lengo la kuvurga kabisa harakati za chama hicho.
Katika taarifa yake iliyotolewa leo (25.09.2013) katika mtandoa wa
facebook, chama cha Udugu wa Kiislamu kimesema "Sisi waandishi habari wa
gazeti la Uhuru na Haki tunalaani kitendo cha vikosi vya usalama
kufunga makao makuu ya gazeti".
Usiku wa kuamkia leo, jeshi la polisi lilizishambulia ofisi hizo na
kuondoa nyaraka kadhaa zilizokuwemo.
Chanzo kimoja kutoka katika kitengo
cha usalama cha Misri kimesema hatua hiyo inatokana na uamuzi wa
mahakama wa Jumatatu, wa kupiga marufuku chama hicho na kuamuru
kudhibitiwa hazina yake.
Mfuasi wa chama cha Udugu wa Kiislamu
Akiendeleza kutoa ufafanuzi kuhusu namna wanavyoendesha
operesheni hiyo chanzo hicho kimesema uamuzi wa mahakama ambao
umesababasha kutekelezwa kwa hatua hiyo kunatokana na kuwepo kwa
mashitaka ya kuchochea vurugu pamoja na vitendo vya ugaidi kulikoteka
katika siku za hivi karibuni.
Mwezi Julai mwaka huu, jeshi lilimuondoa madarakani rais Mohamed Mursi
ambapo pia chama chama chake cha Udugu wa Kiislamu kimeshuhudia mikasa
ya mamia ya wanachama wake kuuwawa na wengine maelfu kukamatwa tangu
wakati huo.
0 comments:
Post a Comment