HII NI SIKU YA UZINDUZI
Leo ni siku ya mia moja tangu na kuzinduliwa Blog ya Munira Madrasa yenye makazi yake Magomeni Makuti Jijini Dar es salam ambapo wadau mbalimbali wamejitokeza na kuipongeza.
Blog hiyo inayomilikiwa na Muniira Madrasa And Islamic Propagation Association ilizinduliwa tarehe 01/06/2013 na waziri wa Habari,Utalii Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Said Alli Mbarouk,ambaye alikuwa anamuwakilisha Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzabar Mhe Maalim Seif Sharif Hamad.
Akisoma risala katika uzinduzi wa blog hii,Katibu Mkuu wa Muniira madrasa Alhaj Juma Rashid ambaye pia ni Mkurugenzi wa blog hii alisema,"tunakiri na kufahamu uwepo wa vyomba vya habari vya Kiislamu,na tunaunga mkono uwepo huo,lakini tumeona bado kuna hitajio kubwa zaidi la kupanuwa wigo wa uwepo wa vyombo vya habari vya Kiislam ili Waislamu wapate fursa pana ya kupata habari zao na za kijamii kwa sahihi na kwa uwazi zaidi"
kwa upande wake mhe Said Alli Mbarouk kwa niaba ya makamu wa rais alisema Serikali ya mapinduzi zanzibar imefurahishwa mno na hatua ya munira madrasa na ikaahidi kuiunga mkono.
kufuatia leo hii kutimiza siku mia moja tangu kuzinduliwa blog hii,tulifanya mahojiano na wadau kadhaa wa habari na kutoa maoni yao kama ifuatavyo:
kwa upande wake mhariri wa habari wa kituo cha channel ten said mhiko alisema "Nimeipitia blog yenu,kwa hakika muko vizuri ila si vibaya tukionana kwa ajili ya kubadilishana mawazo"
Abaas Al Sabry mtangazaji wa Redio Kheri alisema "mumefanya kitu ambacho wengi hawakukifikiria,kwani blog nyingi zimeanzishwa na wana habari,lakini nyinyi ni madrasa ya kawaida tu na mumeanzisha kitu kama hiki,kwa hakika mumeleta mapinduzi makubwa katika madrasa hapa nchini ila mufahamu blog zinaushindani mkubwa sana,sasa mukaze buti."
Ndugu Maneno ambaye ni mwandishi wa Gazeti la Mtanzania alisema,nimeipitia na nimefurahishwa sana na ubunifu wenu,musisite kuhitaji mchango wangu ikibidi'.
"Ninaipitia blog yenu kila wakati,tena naridhika na juhudi zenu,ila ninasafari nikirudi salama tuonane Inshaa Allaah ,lakini mupo vizuri sana ndani ya kipindi hiki kifupi mulichoaanza,alisema Juma Mmanga ambaye ni afisa mnadhimu wa vyombo vya habari vya serikali ya mapinduzi ya zanzibar
kwa upande wake Bakari Mwakangwale Mwandishi wa Gazeti la Annur alisema "inafaa tuonane ili tuboreshe zaidi,kwani kuna hitajika kufanya hivyo".
Sheikh Omar Al had Imamu wa Msikiti wa Kichangani amesema "Jamii ya Kiislamu inalazimika kuunga mkono harakati zenu kwani hii ni hatua kubwa itakayowafaidisha Waislamu na jamii nzima ya Watanzania kwa kupata habari zilizo makini,haya ndiyo mabadiliko tunayoyahitaji,ustaadh najuwa mnakabiliwa na changa moto nyingi na ninafahamu juhudi zenu kwa kipindi kirefu sana lakini musikate tamaa,mutafanikiwa Inshaa Allah",mwisho wa kumnukuu.
PICHA CHINI SEHEMU YA WANA HABARI WAKIWA KAZINI.
HII NI SIKU YA UZINDUZI
munirablog inawashukuru wasomaji na wadau wote kwa kutuunga mkono na kutupa moyo wa kukitumikia chombo hiki,ila tunaomba kwa wenye nafasi kutusaidia kamera na vinasa sauti (siyo pesa) kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa kazi zetu,kwani hadi sasa tuna kamera moja na lap top moja tu kitu ambacho kinatupa uzito wa kufuatilia na kuandaa habari.
Wasiliana nasi kwa simu no 0719 46 47 00
0786 46 47 00
0713 441 639
0658 316 316
0 comments:
Post a Comment