Dosari kadhaa zilizojitokeza katika mchakato wa muswada wa sheria ya mabadiliko ya uchaguzi yaliyotokea hivi karibuni Bungeni yameelezwa kuwa ni hujuma za makusudi dhidi ya Rais Kikwete.
Hayo yamesema mwishoni mwa wiki na Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni Mhe Habib Mnyaa alipokuwa anawahutubia maelfu ya wananchi waliofurika katika viwanja vya Jangwani katika mkutano ulioandaliwa na vyama vya upinzani ikiwa ni kupinga muswada wa marekebisha ya sheria uliopitishwa bungeni hivi karibuni.
"Ndugu zangu kwanza naomba ifahamike,miaka kumi na mbili iliyopita Chama Cha Wananchi (CUF) kilifanya maandamano makubwa ya kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,katika maandamano yale Jeshi la Polisi liliwauwa wanachama 32 wa CUF,tunamshukuru mungu,maandamano yale yamazaa matunda baada ya Rais Kikwete kuridhia uwepo wa mchakato wa mabadiliko ya katiba japo wana CCM wenzake walimpinga"
Aliendelea kusema kwamba "lakini kuna hujuma za wazi wazi zinafanywa na watendaji wake kwa lengo la kukwamisha nia njema ya Rais kikwete,kwa mfano tukio lililotokea Bungeni Dodoma la kumzuwia na kumtoa nje kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe ni tukio linalopingana na mabunge ya jumuiya ya madola na sisi Tanzania ni sehemu ya jumiya ya madola,mbali ya hayo bunge la katiba kuwa na wajumbe wachache kutoka Zanzibar wakati tume ya Jaji Warioboa ina wajumbe idadi sawa wanaotoka Zanzibar na wa huku Bara,haya na megineyo ni dhahiri ya kwamba ni HUJUMA dhidi ya Rais kikwete"mwisho wa kumnukuu.
Aidha Mhe Mnyaa alipinga suala zima la kuidharau Zanzibar na kusema hawatoruhusu hali hiyo iendelee.
Huku akitoa mfano kwa mujibu wa katiba vikao vya kamati za bunge vinaweza kufanyika zanzibar (alinukuu ibara mbalimbali) lakini havijawahi kufanyika Zanzibar hata siku moja licha kuwa na ukumbi wa kutosha badala yake vikao hivyo vinafanyika Dar es alaam na wanakodi kumbi mbalimbali baada ya kuwa ukumbi wao ni mdogo,huku ni kufuja kodi za wananchi alisema.
HAWA NI AKINA MAMA WAKISHIRIKI MKUTANO HUO WAKIWA WAMEJISTIRI VIZURI
PROFESA LIPUMBA AKIWA AMEMBEBA MLEMAVU AMBAYE KWA KIPINDI KIREFU ALIONEKANA KUWA NA HAMU YA KUKUTANA ANA KWA ANA NA PROFESA LIPUMBA.
MOTOOO;NDIVYO WANAVYOITIKIA WANANCHI
0 comments:
Post a Comment