Taasisi ya DYCCC ya jijini Dar es salaam kupitia Idara ya Madrasa ,inakusudia kuwapatia Semina Waalimu Wa Madrasa wa mkoa wa Dar es salaam.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Idara hiyo Sheikh Omar Awadh alipokuwa anazungumza katika mkutano maalumu baina ya uongozi na waalimu hao.
Amesema "idara yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia waalimu wa madrasa kwa kadri tunavyoweza,nakiri ya kwamba munahitaji misaada mingi na ya aina mbalimbali lakini tumepanga kuwapatia semina kumi na mbili (12) ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kutoka sasa tunaamini hii itawasaidia sana"
Aliendelea kusema "Semina hizo zitahusisha elimu ya uongozi,utawala,udhibiti wa fedha,saikoloji n.k kwani tunataka tufike wakati mwalimu wa Qur aan awe na maarifa zaidi ili aende sambamba na teknoloji iliyopo".
Aidha alisema Idara hiyo inakusudia kufungua Blog ili itoe habari mbalimbali za idara hiyo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na waalimu 48.
KATIBU MKUU WA IDARA HIYO SHEKH RAMADHAN KWANGAYA AKIFAFANUA JAMBO.
MMOJA WA WASHIRIKI AKITOA MAONI.
BAADHI YA WALIMU WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MWENYEKITI KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI.
BAADHI YA WALIMU WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MWENYEKITI KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI.
0 comments:
Post a Comment