Sep 26, 2013

Mtoto Ataka Kujiuwa Kupinga Kudhulumiwa

Mtoto Alan Kewa (12) mkazi wa Keko Mwanga amenusurika kifo baada ya kunywa sumu ya panya.

Mtoto huyo alitaka kujiua baada ya kuona anadhulumiwa mali ya marehemu baba yake. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiondo, alisema motto huyo alitaka kujiua Septemba 24 mwaka huu.

Alisema inasadikiwa mtoto huyo alikunywa sumu ya panya ya mice killer akitaka kujiua baada kuona anadhulumiwa mali ya marehemu baba yake.

Aliongeza kwa kusema shangazi yake aliyemtaja kwa jina moja la Barched inadaiwa hajamlipia ada ya shule.
 
Mtoto huyo amelazwa katika Hospitali ya Polisi Barracks kwa matibabu na juhudi za kumtafuta shangazi yake zinaendelea.

0 comments:

Post a Comment