KITUO cha mafuta cha GAPCO kimenusurika kuungua moto.
Kituo hicho kilichopo barabara ya msimbazi jirani na makutano ya mtaa wa swahili kimenusirika na janga hilo majira ya saa tatu na dakika arobaini asubuhi ya leo.
Mkasa huo ulikuja kufuatia mwendesha pikipiki akiwa katika safari zake za kawaida ambaye alipofika katika mlango wa kuingilia kituoni hapo pikipiki yake ikaanza kuungua.
Munirablog ilishuhudia tukio hilo huku mwendesha pikipiki akiiacha piki piki na kukImbilia maji kwa lengo la kuuzima bila mafanikio.
Kufuatia hali hiyo mmoja ya wafanya kazi wa kituo hicho alitoka na kifaa maalumu cha kuzimia moto ambapo ilimchukua takribani dakika sita kufanikisha kuuzima huku kofia ya dereva huyo ikiwa imeungua kabisa.
"Nafikiri hili litakuwa ni tatizo la wirering alisikika mtu mmoja akisema",
Kwa upande wake dereva wa pikipiki hiyo licha ya kutopata madhara hakuwa tayari kuzungumza lolote.
WATU WAKISHUHUDIA AJALI HIYO.
0 comments:
Post a Comment