Taasisi ya jopo la Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu nchini Tanzania imeendaa Sensa ya Misikiti itakayoanza wiki hii.
Akizungumza katika Semina hiyo iliyowahusisha waalimu wa Madrasa,katibu mkuu wa HAY ATUL ULAMAA Sheikh Yasir Salim alisema ,"dhamira ya Sensa hii ni kujuwa hali halisi ya mazingira ya Misikiti yetu nchini Tanzania,hatuwezi kufanya lolote la maendeleo tena kwa ufanisi mkubwa kama hatujajuwa hali halisi ya misikiti yetu"
Aliendelea kusema "tukisha fanya tafiti hiyo itaweza kutusaidia kujuwa mambo mengi ikiwemo viwango vya elimu vya maimamu na makhaatwibu,uchumi na miradi ya misikiti yetu,hali ya usafi na mazingira kwa ujumla,uongozi bora na mengineyo,sasa hapo tutakuwa na fursa ya kuzikabili changamoto zitakazo patikana baada ya tafiti hiyo".
"Leo hakuna mtu anayejuwa idadi kamili ya misikiti yetu,wala hakuna mtu au Taasisi inayojuwa hali halisi ya misikiti ya Tanzania,wala hakuna mtu au taasisi ambayo inaweza kujuwa mawasiliano kamili ya misikiti yetu iliyopo Tanzania,lakini kwa tafiti hii itatuwezesha kujuwa hayo na mengine" mwisho wa kumnukuu
Awali akiongea katika semina hiyo,Sheikh Abdallah Bawazir alisema ingekuwa misikiti inafanya kazi zake kikamilifu,kusingekuwa na haja ya kuwa na balozi wa nyumba kumikumi.
kwa bahati mbaya hilo halipo kabisa na ni kinyume na mfumo wa uislamu.
Aidha alitowa wito kwa misikiti kuweka kumbukmbu (nyaraka) kikamilifu.
"Tumekuwa tunaswali na madaktari,mahafidhul Qur aan na watu wenye fani na elimu mbalimbali,lakini hatuwajuwi na hatuwatumii kwa kuwa hatuna utamaduni wa kuchukuwa historia za waumini wetu,matokeo yake madhali mtu ana uwezo wa pesa au uwezo wa kusema sana ndiyo anapewa uongozi katika kamati kumbe historia yake mtu huyu ni ya ujambazi au uhalifu mbalimbali",alisema.
Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa DYCCC uliopo kariakoo jijini Dar es salaam.
HAY ATUL ULAMAA inakusudia kuanza tafiti yake katika misikiti mia tatu iliyopo katika Jiji l Daer esalaam na baadaye katika mikoa mengine.