Aug 17, 2013

MAMIA YA WATU WAFARIKI MISRI

HABARI ZA KIMATAIFA;

Na mwandishi wa BBC,LONDON
Hali imezidi kuwa mbaya katika nchi ya Misri baada ya jeshi la nchi hiyo kuwaondoa kwa nguvu wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Muhamed Morsi waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Tahriri kwa wiki sita mfululizo.

kwa mujibu wa mwanahabari wa BBC anasema wengi wa waathiriwa walifariki dunia katika mji mkuu wa Cairo lakini kulikuwa na vurugu katika maeneo yote ya nchi katika siku iliyoshuhudia umwagikaji mkubwa wa damu tangu mapinduzi ya kidemokrasia yaliyotokea miaka miwili iliyopita.

Idadi kamili inaaminika kuwa juu zaidi kwa kuwa miili mingi ya waliofariki dunia bado haijasajiliwa.

Wafuasi wa rais Mohammed Morsi, aliyeng'olewa marakani mwezi uliopita wanasema zaidi ya watu 2,000 waliuwawa.

Mwandishi wa BBC Khaled Ezzelarab ameripoti kuwa ameshuhudia zaidi ya miili 140 ikiwa imefungwa kwenye sanda katika Msikiti wa Eman, uliopo karibu na kambi ya maandamano ya Rabaa al-Adawiya.

Vugugu la Undugu wa Kiislamu, Muslim Brotherhood, ambalo linamuunga mkono bwana Morsi, linapanga maandamano mengine mjini Cairo na mji wa pili kwa ukubwa, Alexandria, kulalamikia mauaji hayo. 

Tumuombe mungu awanusuru ndugu zetu. 

 HUYU NI MMOJA WA RAIA AKIWA KAPOTEZA NDUGU ZAKE KWA WAKATI MMOJA,NA HIYO PENDENI MWAKE NI MIILI YA WALIOFARIKI WAPATAO 140IKIWA IMESHAVESHWA SANDA


Wakati huo huo
Chama cha Rais aliyetolewa madarakani, Mohammed Morsi, hakikubali juhudi za kupatanisha zinazofanywa na mmoja kati ya viongozi wakubwa wa kidini nchini Misri.

Msemaji wa mashauri ya nchi za nje wa chama cha Bwana Morsi, cha Freedom and Justice Party, aliuliza ikiwa imamu mkuu wa al-Azhar kweli hapendelei upande wowote.
Alisema imamu huyo alipanga njama dhidi ya rais, na aliunga mkono jeshi kumpindua Morsi.
Mohammed Soudan aliongeza kusema kuwa haikuelekea chama chake kuombwa kuzungumza wakati viongozi wake wako jela au wanakabili mashtaka.
Chama hicho ni tawi la siasa la Muslim Brotherhood.
Bwana Soudan piya alionya kuwa maandamano ya wafuasi wa Bwana Morsi yataendelea na kwamba watu wako tayari kufa.

HAWA NI SEHEMU WA WAFUASI WA MORSI WAKIWA KATIKA MAANDAMANO KUPINGWA KUONDOLEWA KWA NGUVU MADARAKANI KWA RAIS WAO WA KWANZA KUCHAGULIWA KWA DEMOKRASI BAADA YA UTAWALA WA KIFALME.

*************************************************************************************************************
 
Mama mmoja akiomboleza baadhi wa watu waliouwawa na jeshi ,Misri



 HAYA NI MAUWAJI YANAYOENDELEA KUFANYWA NA JESHI LA MISRI;INNAA LILLAAH WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN


BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LATAKA UVUMILIFU;
  • MAREKANI YASHUTUMU,SAUDIA ARABIA YAUNGA MKONO,
  • NCHI NYENGINE DUNIANI ZAANDAMANA KUPINGA MAUWAJI.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limefanya mkutano wa dharura kuzungumzia namna vikosi vya usalama vya Misri vilivyowaua wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi na kusema kuna haja ya pande husika kuwa na "uvumilivu wa hali ya juu".
Tamko hilo la baraza la usalma linakuja siku moja tu baada ya watu wapatao 638 kuuwawa wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya waandamanaji wafuasi wa Muslim Bortherhood

Waandamaji hao wamekuwa wakitaka Bwana Morsi aliyeondolewa uongozini arudishwe madarakani
.
Wakati huo huo rais wa Marekani Barack Obama ameshutumu hatua ya serikali ya muda ya Misri akisema haukuwa na sababu za kutosha.
"tunasikitishwa sana na unyama uliofanyiwa raia wa kawaida " , amesema Obama huku akitangaza kuwa zoezi la kijeshi la pamoja kati ya Marekani na Misri ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika mwezi ujao umefutwa.

RAIS OBAMA ALIPOJITOKEA NA KUSHUTUMU MAUAJI HAYO.
Rais Obama amesema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hauwezi kuendelea wakati raia wanauwawa.
Licha ya mauaji hayo na umwakikaji mkubwa wa damu ,lakini kikao hicho cha dharura cha umoja wa mataifa kilichoandaliwa mahusus kujadili swala la Misri kilikumbwa na mgawanyiko mkubwa baina ya wanachama 15 wa baraza hilo la Usalama.
Wanachama hao 15 walishindwa kuafikiani kuhusu jinsi ya kukabiliana na hali ya Misri, huko jeshi likizidi kukaza kamba.
Kwa kawaida Urusi na China huwa zinapinga hatua yeyote ya baraza la usalama kuingilia maswala ya ndani ya nchi yeyote ile. Hivyo katika kikao hicho cha dharura , Urusi na China hazikibadili msimamo wao wa jadi , bado walipinga kuwa Misri na jeshi lisiingiliwe bali njia ya maridhiano itafutwe.
Pengine hii ni kutokana na swala la Chechnya ambalo bado linaisumbua Urusi huko China ikihangaishwa na tatizo la Tibet.
Taarifa zinasema China ilikataa katakata kutia saini taarifa rasmi ya baraza la usalama la kulishutumu jeshi la Misri kwa kusababisha umwagikaji wa damu na mauaji.

Kwa upande mwengine wakati blog ya munira inakusanya habari,imeelezwa kwamba mfalme Abdu Azizi wa Saudia ameunga mkono Jeshi la misri kumuondoa kwa nguvu madarakani aliyekuwa Rais wa misri Muhamad Mors,

Wakati hayo yakijiri mataifa mbalimbaliduniani yanaadamana kupinga unyama unaofanywa na jeshi la nchi ya misr,miongoni mwa nchi hizo ni Jordan na Indonesia.