Aug 18, 2013

WAISLAMU WATOA TAMKA


SAKATA LA SHEIKH PONDA
·        WAIKATAA TUME YA POLISI,WATAKA TUME HURU,
·        KAMANDA SHILOGILE NA WENZAKE WASHITAKIWE
·        WAZIRI NCHIMBI ATAKIWA KUJIUZULU.

Na mwandishi wetu wa munira;
Hatimaye Waislamu nchini Tanzania wametoa Tamko kufuatia tukio la kikatiri la kupigwa risasi Sheikh Ponda Issa Ponda  mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hayo yamesemwa jioni hii na Sheikh Kondo Juma Bungo alipokuwa akizungumza na maelfu ya Waislamu waliofurika katika viwanja vya Mwembe Yanga vilivyopo Tandika Jijini Dar salaam.

Amesema Sheikh “Ponda Issa Pondo hakupigwa risasi kwa bahati mbaya,Serikali inayoongozwa na CCM ilidhamiria kumpiga risasi Sheikh Ponda na lengo lao lilikuwa ni kumuuwa lakini kwa Rehma za ALLAAH Sheikh Ponda amenusurika labda wammalizie huko alipo”mwisho wa kumnukuu.

Ndugu Waislamu kwa nini nasema walikusudia,taratibu za kumkamata kiongozi awe wa dini au wa kisiasa zipo wazi,mbali ya hayo nyumbani kwake wanapajuwa,lakini kwa kuonesha kwamba walikusudia,vituko vyao vilianza siku ya Iddi mosi mimi na Sheikh Ponda tulikuwa ni miongoni mwa tulioshiriki katika Baraza la Idd pale Kichangani,tukiwa ndani ya Baraza la Idd,tukapigiwa simu kutoka Jeshi la polisi kwamba marufuku Sheikh Ponda kuongea,tukajiuliza kwa nini asiongee,sisi tukasema lazima aongee na aliongea”alisema

Sheikh Kondo aliendelea kuuzindua umma kwa kusema “mara baada ya Baraza la Idd kumalizika,jioni ile ile tukaenda Morogoro mimi,Sheikh Ponda na dereva wetu.Viongozi wa Waislamu wa Mkoa wa Morogoro wakaomba kibali Jeshi la Polisi na wakaruhusiwa,tukiwa ndani ya Mhadhara tukaletewa taarifa kutoka Polisi kwamba Sheikh Ponda asiongee,mara tukaona vikosi vya Usalama vinazidi kuongezeka,tulipo maliza na kuanza kuondoka magari ya polisi yakaanza kutufuata,nikakubaliana mimi na Sheikh Ponda ambao tulikuwa viti vya nyuma ya kwamba hawa wamekusudia shari,sasa kila mtu aangalie namna ya kufanya.Nikiwa umbali wa mita mia moja nikapata taarifa ya kwamba Ponda kapigwa risasi”

Ndugu zangu tukiangalia Historia ya huko tulipotoka inaonyesha kwamba hii Serikali ya CCM kupitia Jeshi la Polisi wanatabia ya kuua hovyo hasa kwa waislamu,sasa wamekusudia kutumaliza sisi waislamu wakiamini kwamba hiyo ndiyo njia ya kutuzuwia tusiyaweke wazi madai yetu,lakini napenda wafahamu kwamba japo Sheikh Ponda hajafa lakini damu yake ni lazima ilipwe,na hata wakimuua Sheikh Ponda lakini hatutorudi nyuma na tutazidi kufichua dhulma tunazofanyiwa waislamu”.

Akitoa msimamo wa Wasilamu Sheikh Kondo alisema “Tunaitaka Serikali ifanye mambo matatu,Iunde tume huru itakayochunguza kadhia hii kwa uadilifu na uwazi (hatuitaki wala kuitambua tume iliyoundwa na Jeshi la polisi).
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile afikishwe mahakamani yeye na kiongozi wa Opresheni katika tukio hilo.
 Waziri wa ulinzi Mhe Nchimbi naye ajiuzulu.

 HILI NDILO JERAHA LA RISASI KATIKA MWILI WA SHEIKH PONDA.
 
 TAKBIIR,WAISLAMU WAKISIKILIZA TAMKO WAKATI SHEIKH KONDO AKIWASILISHA TAMKO HILO JIONI HII.