Aug 17, 2013

SAKATA LASHEIKH PONDA; WAISLAMU NJOONI MWEMBE YANGA-SHEIKH KUNDECHA

  • POLISI WAALIKWA NA WATAKIWA KUACHA PROPAGANDA.
  • KUNDECHA AKANUSHA KUITISHA MAANDAMANO

Na mwandishi wetu wa munirablog;
Waislamu wa mkoa wa Dar es salam na wa pembezoni mwake wametakiwa kufika kwa wingi katika uwanja wa Mwembe Yanga uliopo Tandika Manispaa ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam siku ya Jumapili (kesho) ya tarehe 18 augosti .

Wito huo umetolewa jana na Amir wa Shuura ya Maimamu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza kuu Sheikh Mussa Kundecha alipokuwa akizungumza na waislamu katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni Mapipa.

"Niliitwa na Jeshi la Polisi wakaniaambia kwamba eti wamepata taarifa ya kwamba mimi  jana (juzi) katika msikiti huu niliwatangazia Waumini kwamba leo Ijumaa baada ya Swala ya Ijumaa kutakuwa na maandamano,kwa kweli niliwashangaa mimi sikuwepo hapa juzi kwa muda huo waliousema wao,na wala sijatangaza wala kuratibu maandamano hayo,ila sasa nawaalika wao polisi,nawaalika wana habari ya kwamba Siku ya Jumapili waje mwembe yanga pale tandika kutakuwa na mkutano mkubwa sana wa Waislamu ambao utatowa taswira mzima ya kadhia ya Sheikh wetu (Ponda),tena nawaomba polisi waache tabia ya propaganda"mwisho wa kumnukuu.

Jana Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi mkali katikati ya Jiji na hasa katika baadhi ya misikiti kwa kuhofia kufanyika maandamano ya Waislamu kupinga dhulma anayofanyiwa Sheikh Ponda ambaye kwa sasa anasota katika gereza la Segerea baada ya tarehe 14 augost kusomewa mashtaka ya uchochezi akiwa kitandani katika wodi ya taasisi ya mifupa (MOI) na siku iliyofuata kuchukuliwa na kupelekwaSegerea,"unajuwa hawa wanakiogopa kivuli chao wenyewe wanajuwa walichokifanya "alisikika akisema mtu mmoja jana bila kufafanua alipoona msafara wa mapikipiki ya polisi yakitoka katika kituo cha msimbazi kariakoo.