Jul 19, 2013

WALINGANIAJI TUBADILIKE.SHEIKH MUHAMMAD IDD



Na mwandishi wetu wa munira.



Wahadhiri wa Kiislamu wametakiwa kubadili mbinu za kuwalingania watu ili kukabiliana na changamoto zilizopo.

Ushauri huo umetolewa jana usiku na Sheikh Muhammad Idd Muhammad alipokuwa akiendesha kipindi chake cha RAMADHAN KARIIM kinachorushwa LIVE kupitia kituo cha CHANNEL TEN cha Jijini Dar es salaam.

Amesema kumekuwa na wimbi kubwa la Waumini wa Kiislamu kujaa Misikitini katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhan lakini mfungo huu ukiisha na baadhi ya waumini wanaondoka na misikiti kubaki na waumini wachache,haya yanatokea wakati kila kukicha wahadhiri wanawatahadrisha waumini juu ya madhara ya kutokuswali au kufanya ibada kwa ujumla.

"Natoa wito kwa madai (walinganiaji)  kwamba sasa tubadilshe mbinu,badala ya kuzungumza sana adhabu za watu kwa kutokuswali basi sasa tuzungumze sana malipo mema watakayo yapata wenye kuswali na kufanya ibada kwa ujumla,inawezekana wakavutiwa na haya",alisema

 
 SHEIKH MUHAMMAD IDD AKIZUNGUMZA KUPITIA KIPINDI CHAKE CHA RAMADHAN KAREEM KINACHORUSHWA LIVE NA KITUO CHA CHANNEL TEN