Jul 20, 2013



MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR AAN KUFANYIKA KESHO.

  • NI KATIKA UKUMBI WA DIOMOND JUBILEE,

  • YAMEANDALIWA NA AISHA SURURU FOUNDATION,

  • KIVUTIO KIKUBWA NI KWA WATOTO WALEMAVU WA MACHO.

Na mwandishi wetu wa munirablog
Taasisi ya Aisha Sururu Foungation ya Jijini Dar es salaam,imeandaa mashindano ya kuhifadhi Qur aan kwa watoto yatakayofanyika kesho Inshaa Allah.

Akiongea kwa njia ya simu na munirablog,Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo Bi Aisha Sururu amesema mashindano hayo yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee uliopo upanga Jijini Dar  es salaam kuanzia saa mbili Asubuhi hadi saa saba Adhuhuri.

Amesema wanafunzi kutoka mikoa saba ya Tanzania bara na kutoka visiwani Zanzibar watashiriki.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na mkoa Dare s salaa (mwenyeji wa mashindano hayo) Tanga,Arusha,Morogoro,Dodoma,Pwani na wanafunzi kutoka Kisiwa cha Mafia.

Aliendelea kusema “pia kutakuwa na wanafunzi kutoka visiwani Zanzibar ambapo kuna watoto watano walemavu wa macho kutoka Pemba nao watashiriki,nawaomba Waislamu waje kwa wingi kuona vipaji vya ajabu vya watoto hawa”,mwisho wa kumnukuu.





0 comments:

Post a Comment