Mar 15, 2016

Haya ndio yaliyotokea usiku wa kuamkia leo Pemba.

 10464141_1176213469064368_2876723535492258797_n


Hali inazidi kuwa tete baada ya wanaodaiawa kua ni Askari wa CCM wakiwa na mazombi kutembeza mkongo'oto kwa baadhi ya wananchi  usiku wa kuamkia leo.

kwa mujibu wa mashuhuda wametupasha kwamba tukio hilo limetokea wete pemba baada ya wanaotajwa kuwa ni walinzi wa maskani kukaidi agizo la mkuu wa mkoa la kutotembea baada ya saa mbili usiku.

"Kilichotokea ni mtoto wa Bin Haroub ambaye ni CCM usiku wa kuamkia Leo askari wa CCM wakiwa pamoja na Mazombi’ wamemchapa vibaya vibaya kwa kukaidi agizo la Mkuu wa Mkoa, kosa kujifanya walinzi wa maskani yao mjini Wete Pemba wakisahau kwamba mwisho ni saa mbili usiku kukaa nje Mkoa wa Kaskazini' mwisho wa kumnukuu shuhuda huyo ambaye hakutaka jina lake wala picha yake itumike.


0 comments:

Post a Comment