Mar 12, 2016

Algeria yapinga kutajwa Hizbullah kuwa kundi la kigaidi

Algeria yapinga kutajwa Hizbullah kuwa kundi la kigaidi
Algeria kwa mara nyingine imepinga uamuzi wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu kuitajwa Hizbullah kuwa kundi la kigaidi. 
 
Abdulqadir Masahil Waziri wa Mashauri katika masuala ya Eneo la Maghreb, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amepinga hatua ya kutajwa Hizbullah kuwa kundi la kigaidi. Amesema uamuzi huo unakinzana na kanuni za kimataifa. 

Waziri huyo wa Algeria ameashiria nafasi ya kitaifa, kisiasa na kijamii ya Hizbullah nchini Lebanon na kusema, Algeria inazingatia msingi wa kutoingilia masuala ya nchi zingine katika sera zake za kigeni. Aidha amesema Algeria inataka migongano iliyopo katika eneo itatuliwe kwa njia za amani na mazungumzo. 

Waziri huyo wa Algeria amesema mazungumzo baina ya pande hasimu Yemen yatatuliwe kwa mazungumzo ili uthabiti urejee katika nchi hiyo. 

Ikumbukwe kuwa siku ya Ijumaa, nchi za Jumuiya ya Kiarabu katika kikao cha Cairo zilitangaza kuwa eti Hizbullah ni kundi la kigaidi. Uamuzi huo ulipingwa vikali na Algeria, Lebanon na Iraq.

0 comments:

Post a Comment