Mar 8, 2016

"Tuhuma za Cairo kwa Ikhwan na Hamas ni uongo"

"Tuhuma za Cairo kwa Ikhwan na Hamas ni uongo"
Msomi na mwandishi maarufu wa Misri, Fahmi Huwaidi amesema kuwa, tuhuma zilizotolewa hivi karibuni za Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo dhidi ya harakati ya Ikhwanul Muslimin na harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, ni kichekesho.

Huwaidi amesema kuwa, Wamisri kwa ujumla wanaziona tuhuma za serikali ya Cairo dhidi ya harakati hizo na madai kwamba zilihusika na mauaji ya mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Hisham Barakat, kuwa ni kichekesho na maskhara. 

Msomi huyo ameongeza kuwa, tuhuma hizo za Cairo hazina msingi na ni za kubuni. Amesisitiza kuwa, polisi ya Misri imethibitisha kufeli kwake katika kuwatambua wahusika wa jinai hiyo suala ambalo imeilazimu Cairo kuzituhumu harakati hizo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Ikhwanul Muslimin imekanusha tuhuma zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kuwa wanachama wa kundi hilo walihusika na mauaji ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi hiyo mwaka jana. 

Hisham Barakat, aliuawa mwezi Juni mwaka jana akiwa ndani ya gari baada ya kulipukiwa na bomu katika eneo la Heliopolis nchini humo.

0 comments:

Post a Comment