Mar 8, 2016

Mhubiri wa US awanyanyasa kingono wafungwa Kenya

Mhubiri wa US awanyanyasa kingono wafungwa Kenya
Mhubiri Mkristo wa Marekani amehukumiwa miaka 40 jela kwa kuwanyanyasa kingono watoto katika kituo kimoja cha mayatima chini Kenya.

Mahakama moja ya Marekani imesema Matthew Lane Durham mwenye umri wa miaka 21, alifanya''kitendo hicho kiovu dhidi ya watoto wasioweza kujitetea''.

Durham aliwalenga watoto mayatima alipokuwa akifanya kazi ya kujitolea katika kituo cha mayatima cha Upendo Childrens Home katika mji wa Juja eneo la kati mwa Kenya Aprili na mwezi Juni 2014.

Mwaka jana watoto watano walionyanyaswa kijinsia walisafiri kutoka Kenya kuelekea Marekani ambapo walitoa ushahidi katika kesi ya Durham na ushahidi wao ulisikizwa katika kikao cha faragha. Mbali na kifungo cha miaka 40, mahakama pia iliagiza kwamba Durham alipe dola 15,863.

Hii si mara ya kwanza kwa raia wa nchi za Magharibi wanaowakilisha mashirika ya misaada kupatikana na hatia ya vitendo vya uhalifu wa kingono dhidi ya watoto nchini Kenya. 

Mwaka uliopita, Simon Harris mwenye umri wa miaka 55 alihukumiwa kifungo cha miaka 17 jela na mahakama ya Uingereza kwa kuwanyanyasa watoto kati ya mwaka 1996 na 2013 katika mji wa kilimo wa Gilgil katika eneo la Rift Valley.

0 comments:

Post a Comment