Watu 34 wanaripotiwa
kuuawa katika kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya watu
waliokuwa na silaha kufanya mashambulio katika kijiji kimoja.
Afisa
mmoja wa vikosi vya kusimamia amani vya Umoja wa Afrika katika Jamhuri
ya Afrika ya Kati MISCA ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema
kwamba, watu wengine kumi wameuawa katika shambulio hilo.
Taarifa zaidi
zinasema kuwa, shambulio hilo limetokea kilomita 400 kaskazini mwa mji
mkuu Bangui. Wakati huo huo, Askofu Mkuu wa Bangui, mji mkuu wa Jamhuri
ya Afrika ya Kati ametoa wito wa kuharakishwa mchakato wa kuundwa
serikali mpya sambamba na kuongezwa juhudi za kuhitimisha masaibu
yanayowakabili wananchi wa nchi hiyo.
Dieudonne Nzapalainga
amesisitiza kwamba, kuna haja ya kuchukuliwa hatua za haraka za
kuhitimisha mgogoro wa nchi hiyo.
Kushtadi mapigano ya kikabila baina ya
makundi ya wanamgambo tangu mwezi Disemba mwaka jana kumeifanya Jamhuri
ya Afrika ya Kati kuwa nchi ya machafuko na isiyo na amani huku
Waislamu wakiwa waathirika wakubwa zaidi wa machafuko hayo.
0 comments:
Post a Comment