Ndege na vifaru vya utawala haramu wa Kizayuni zimeanzisha tena
wimbi la mashambulizi dhidi ya Ukanda wa Ghaza baada ya kumalizika
muhula wa usitishaji vita wa masaa 72.
Maeneo kadhaa ya ukanda huo leo yameshuhudia mashambulizi ya Wazayuni yaliyopelekea kwa uchache mtoto mmoja wa miaka 6 kuuawa shahidi na watu kadhaa kujeruhiwa.
Utawala wa Kizayuni umetangaza kuwa, umeanzisha mashambulizi hayo baada ya kumalizika muda wa masaa 72 na kushindikana kuongezwa muda usitishaji vita huo. Kwa upande wake muqawama umejibu mashambulizi hayo kwa kuvilenga vitongoji kadhaa vya walowezi wa Kizayuni na kufanya walowezi wengi kukumbwa na wahka mkubwa sanjari na kupigwa ving'ora vya hatari katika miji mingi ya Israel. Hii ni katika hali ambayo Fauz Barhum, Msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS asema kuwa, makundi ya muqawama ya Palestina, yamepinga kuongezwa muda wa usitishaji vita na utawala wa Kizayuni, kutokana na Israel kushindwa kutekeleza masharti yao ikiwemo kuacha kuuzingira ukanda huo.
Katika upande mwingine, viongozi wa Misri leo wameruhusu kufunguliwa kivuko cha Rafah kwa lengo la kupitisha majeruhi wa Ukanda wa Ghaza kwenda kutibiwa nchini humo.
Viongozi wa serikali ya Cairo wametangaza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kwa ajili tu ya kuwaruhusu majeruhi na kwamba hadi sasa bado mawasiliano ya kina yanaendelea kuhusu suala hilo.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa hadi sasa ni majeruhi 500 pekee waliokwishavuka katika kivuko hicho, tangu yalipoanza mashambulizi ya kinyama ya utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
Hii ni katika hali ambayo serikali ya Cairo ilikuwa imekataa kufungua kivuko hicho na hivyo kufanya hali ya mambo kuwa mbaya zaidi kwa wakazi wa Ukanda wa Ghaza.
Aidha Misri imetangaza kuwa, misaada ya kibinaadamu na tani saba za madawa na zana za kitiba zimeruhusiwa kuingia huko Ghaza mapema jana Ijumaa.

0 comments:
Post a Comment