Aug 9, 2014

A/Kusini kuwafunga jela raia wake watakoisaidia Israel

Viongozi wa serikali ya Afrika Kusini wametishia kuwa, watamchukulia hatua kali ikiwemo kumfunga jela raia yeyote wa nchi hiyo atakayebainika kuhudumu katika jeshi la utawala haramu wa Kizayuni.
Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imetangaza kuwa, raia wa nchi hiyo haruhusiwi kwa aina yoyote ile kuhudumu au kutoa msaada kwa jeshi la Kizayuni hasa katika vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza. 

Onyo la viongozi wa Afrika Kusini, linawahusu pia askari wa nchi hiyo wanaohudumu nchini Afghanistan, na magharibi mwa Afrika. 

Kwa mujibu wa viongozi hao, mtu atakayethibitika kutoa msaada wowote kwa jeshi la Wazayuni basi atahukumiwa adhabu ya kifungo jela. 

Hii ni katika hali ambayo awali serikali ya Pretoria ilichukua hatua kali za jinai za utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya raia wasio na hatia wa Ukanda wa Ghaza. 

Juzi pia Waziri wa Elimu ya Juu nchini Afrika Kusini, Blade Nzimande alisema kuwa, uhuru wa Waafrika Kusini hautakamilika, madhali Wapalestina hawajapata uhuru wao kutoka katika makucha ya Wazayuni.

0 comments:

Post a Comment