Raia wasiopungua 23 wa Palestina wameuawa mapema leo katika
shambulizi lililofanywa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel dhidi ya
shule moja ya Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Ghaza.
Shambulizi hilo limefanywa na ndege za kivita za Israel katika shule ya Wakala wa Umoja wa Mataifa kwa Ajili ya Misaada kwa Wapalestina (UNRWA) katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia ambako mamia ya familia za Kipalestina zimekimbilia hifadhi ya kujikinga na mauaji yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel dhidi ya raia wa Ghaza.
Watu walionusurika na shambulizi hilo wamesema ndege za kivita za Israel zilishambulia shule hiyo ya Umoja wa Mataifa kwa makombora mawili mapema asubuhi wakati raia hao walipokuwa wamelala.
Vyombo vya hospitali katika eneo la Jabalia vinasema raia wengine karibu mia moja wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.
Hii ni mara ya tatu kwa jeshi la utawala katili wa Israel kushambulia shule za Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Ghaza tangu utawala huo uanzishe mashambulizi ya kinyama dhidi ya raia wa eneo hilo zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Ukanda wa Ghaza jana Jumanne ulishuhudia mauaji makubwa zaidi kuwahi kufanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel katika mashambulizi yake ya sasa katika eneo hilo kwa kuuawa Wapalestina 140 zikiwemo familia kadhaa ambazo watu wake wote wameuawa.

0 comments:
Post a Comment