Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa
wafungwa wengi na raia wameuliwa katika mchafuko ya wiki mbili huko
Sudan Kusini.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini (UNMISS)
kimesema kuwa kimehesabu idadi kubwa ya viwiliwili na kwamba ukatili
unaendelea kutokea nchini humo.
UNMISS imesema mauaji ya kiholela dhidi
ya raia na wanajeshi waliokamatwa mateka yametokea katika maeneo tafauti
ya Sudan Kusini kutokana na kuweko ushahidi wa kugunduliwa viwiliwili
vingi vya wahanga wa ukatili huo huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini na
pia huko Malakal na Bor, miji mikuu ya majimbo ya Nile ya Juu na
Jonglei.
Hilde Johnson Mwakilishi wa Umoja wa
Mataifa huko Sudan Kusini pia amelaani ukatili huo uliotekelezwa dhidi
ya raia wa jamii tafauti na wapiganaji wa pande zote mbili zinazohusika
katika mgogoro wa sasa wa Sudan Kusini.
0 comments:
Post a Comment