Jul 28, 2014

MHE PINDA AWAFUTURISHA WAISLAMU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alipowasili kwenye makazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda (nyuma yao) Oysterbay jijini Dar es Salaam kwa ajili ya futari Jumamosi Julai 26, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na wa pili kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova


 Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakijumuika na waumini wengine katika Swala ya Magharibi katika  makaazi ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda Oysterbay jijini Dar es salaam alikoandaa Futari leo Jumamosi Julai 26, 2013
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na baadhi ya waalikwa kwenye futari aliyoandaa, wakiwemo waigizaji Mpoki wa Ze Komedy, Stephen JB, na watangazaji wa redio

 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida wakipakua futari
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akijumuika na waalikwa wengine kupakua futari
 Mawaziri wakuu Wastaafu Mzee Cleopa Msuya na Jaji Joseph Sinde Warioba wakiwa wameketi pamoja na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu (kulia, mwenye baraghashia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio
  Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova (kushoto) akiwa na viongozi wa dini Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar, Lusekelo Antony 'Mzee wa Upako' (wa pili kushoto),  Rais wa shirika la kidini la Wapo Mission International Bishop Sylvester Gamanywa (kulia) na mashehe 
 Meza kuu ikifurahia jambo baada ya futari
 Meya wa jiji la Dar es salaam Dkt Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah Bulembo wakiwa na waalikwa wenzao kwenye futari hiyo
 Sehemu ya waalikwa
 Wazee Mashuhuri wa mkoa wa Dar es salaam mezani pao
 Mufti wa Tanzania Sheikh Shaaban Issa Simba akiongoza dua baada ya futari
 Sehemu  ya waalikwa kwenye futari hiyo
 Rais Kikwete akiagana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Mkowa wa Dar es Salaam
 Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisalimiana na waalikwa baada ya kufuturu pamoja
 Rais Kikwetena  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal wakisalimiana na waalikwa 
 Rais Kikwetena Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakisalimiana na waalikwa baada ya futari
 Rais Kikwete akisalimiana na mchora katuni maarufu Ali Masoud 'Kipanya' huku Mrisho Mpoto akisubiri zamu yale
 Rais Kikwete akifurahi pamoja na waalikwa wenziye
 Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wazee mashuhuri wa Dar es Salaam
 Rais Kikwete akisalimiana na mwanamuziki Christian Bella
 Rais Kikwete akisalimiana na mwanahabari mkongwe Bw. Mwondosha Mfanga
 Rais Kikwete akisalimiana na mwanamuziki nyota wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz

 Rais Kikwete akiongea na Mwana FA
 Rais Kikwete akisalimiana na mtayarishaji, Muongozaji na mwigizaji nyota wa filamu Kulwa Kikumba 'Dude'
Rais Kikwete akiendelea kusalimiana na waalikwa wenziye
Mkono wa mwisho ni wa mtoto huyu aliyepata bahati ya kuagana na Rais Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali baada ya futari

0 comments:

Post a Comment