Jul 30, 2014

MATENDO YA WAISLAMU YASIFANANISHWE NA UISLAM;SHEIKH WA MKOA

 

sababu tunatofautiana imani na wala si dini ya kigaidi…kuna Uislamu na Muislamu na matendo maovu ya Muislamu, yasifananishwe na Uislamu,” alisema Shekhe Alhad katika swala hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Shekhe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba.
Alisema Mtume Muhamad (SWA) aliwafunza Waislamu kuishi na watu wa imani nyingine na kufafanua kuwa mtu ambaye hakukuvurugia amani, mpe amani.

Alisema dunia ya sasa imebadilika kwa kuwa pamoja na kuwa na mafunzo hayo ya kuwatakia amani watu wa dini na imani nyingine, sasa hivi hata watu wa imani moja hawatakiani amani.

Alifafanua kuwa zamani ilikuwa ikisikika watu wa dini mbalimbali wakipigana kama ilivyo sasa katika nchi ya Afrika ya Kati, lakini katika miaka ya hivi karibuni, watu wa mataifa ya Kiarabu, ambao ni watu wa dini moja wamekuwa wakipigana na kumwaga damu.

“Waislamu tunaruhusiwa kuhitilafiana na hivyo ndivyo Mungu alivyotuumba na kutupa akili, lakini si kufarakana,” alifafanua Shekhe Alhad.

Katika hatua nyingine, Shekhe Alhad alizungumzia umuhimu wa umoja katika jamii na kufafanua kuwa katika Uislamu kuna umoja wa aina mbili; umoja wa binadamu na umoja wa Waislamu.

Alifafanua kuwa wanadamu wote wanapaswa kuwa na umoja bila kujali itikadi wala tofauti zao, kwa kuwa wametokana na baba na mama mmoja.  

Kwa mujibu wa Shekhe Alhad, katika kitabu kitakatifu cha Kurani, Mungu amesema amemuumba mwanadamu kutokana na baba na mama mmoja na kuwaweka katika mataifa na makabila mbalimbali.

Alifafanua kuwa kuwekwa katika mataifa na makabila mbalimbali, hakumaanishi taifa au kabila moja kujiona ni la maana kuliko lingine, bali lengo ni kwa mataifa na makabila hayo kufahamiana.

Kuhusu umoja wa Kiislamu, Shekhe Alhad alisema Waislamu dunia nzima wanapaswa kuwa na umoja kama viungo vya mwili na kufafanua kuwa kadhia ya Muislamu mmoja ni kadhia ya Waislamu wote.

Katika ufafanuzi zaidi, Shekhe Alhad alisema kiungo kimoja cha mwili kama kidole kikiumia, mwili wote huuma na hivyo ndivyo umoja wa Wailsamu unavyopaswa kuwa.

Shekhe Alhad alisema Waislamu wengi wamekuwa wakiuawa katika mapigano yanayoendelea kati ya nchi ya Israel na kundi la Hamas, na kuelezea masikitiko yake kuwa mapigano hayo yamefanyika bila hata kukemewa.

Alisema hata makundi ya haki za binadamu, yamenyamaza wakati Waislamu wakiuawa jambo ambalo si jema tena limefanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kusisitiza ni suala la kukemewa.

Aliwataka Watanzania kwa umoja wao, kumuomba Mungu anusuru maisha ya watu wasio na hatia wanaouawa Palestina.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal ametoa mwito kwa Watanzania kulinda amani ili nchi isiingie katika machafuko kama ilivyo katika nchi nyingine ambazo zinavurugu.

Dk Bilal alitoa mwito huo katika ibada hiyo ambapo alisema kwenye Mfungo Mtukufu wa Ramadhani nchi nyingine walikuwa kwenye machafuko.

“Watu wote bila kujali dini zetu tuimarishe upendo, amani na ushirikiano baina ya watu na watu na pia dini zetu mbalimbali na sio kwa Waislamu pekee,” alisema Dk Bilal.

Aliwataka Waislamu kuendeleza mema yote yaliyokuwa yakifanywa na kusisitizwa na viongozi wa dini katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ili kuweka msingi wa mambo mema.

“Kipindi cha Mwezi wa Ramadhani Waislamu tuliishi kwa kumuogopa Mungu na kufanya yale tuliyoagizwa kufanya, mwezi ulikuwa kama darasa kwetu hivyo tuendelee kuishi hivyo hivyo,” alisema Dk Bilal

0 comments:

Post a Comment