Watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa kundi la kitakfiri la Boko
Haram wameshambulia misikiti miwili ya Waislamu wa madhehebu ya Shia
nchini Nigeria na kuua watu wasiopungua 6 waliokuwa wakifanya ibada
katika misikiti hiyo.
Misikiti hiyo miwili iliyopo katika mji wa Potiskum kwenye jimbo la Yobe ilishambuliwa kwa mabomu jioni ya jana Jumanne.
Watu walioshuhudia wamesema mwanachama mmoja wa kundi la Boko Haramu alijilipua kwa bomu katika msikiti wa Thaqafa wakati Waislamu wa madhehebu ya Shia walipokuwa wakiswali Swala la Magharibi na kuua watu wanne katika eneo la Dogo Tebo huko Potiskum.
Shambulizi jingine lilitokea dakika tano baadaye katika msikiti uliopo kwenye eneo la Anguwar Bolawa na kuua Waislamu wasiopungua wawili.
Mji wa Potiskum katika jimbo la Yobe huko Nigeria umekuwa ukikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wafuasi wa kundi la Kiwahabi la Boko Haram japokuwa mashambulizi hayo yamepungua kiasi katika siku za hivi karibuni.

0 comments:
Post a Comment