Wakati
wafuasi wa dini tukufu ya Kiislamu duniani kote wameshaanza kuufunga
mwezi mtukufu wa Ramadhani, Bacary Sagna beki wa timu ya taifa ya
Ufaransa ameeleza kinagaubaga kwamba, ataendelea kufunga saumu ya mwezi
huo, licha ya kukabiliwa na kibarua kigumu cha mashindano ya kombe la
dunia ambayo yameingia hatua ya pili ya mtoano.
Sagna amesisistiza
kwamba, ataendelea kufunga saumu ya mwezi mtukufu, licha ya kukabiliwa
na mechi ngumu kwenye michuano hiyo. Sagna ameviambia vyombo vya habari
vya Ufaransa na hapa tunamnukuu: 'Mimi
nataka kufunga saumu nchini Brazil, kwa kuwa ni Muislamu. Dini tukufu
ya Kiislamu inanipa fursa ya kutofunga saumu nikiwa katika mazingira
maalumu kama vile safari na maradhi, lakini pamoja na kukabiliwa na
mashindano ya kombe la dunia nchini Brazil sitaki kufungulia.
Nitaendelea kufunga saumu ya mwezi mzima wa Ramadhani, Inshaallah',
mwisho wa kunukuu.
Licha ya Bacary Sagna wachezaji wengine wengi
wanaoozichezea timu za taifa za Ufaransa,
Algeria,
Nigeria na Ujerumani wameendelea kusisitiza kwamba watafunga saumu ya
mwezi mtukufu wa Ramadhani licha ya kukabiliwa na mechi ngumu za kombe
la dunia. Hapo kesho, Nigeria 'Tai wa Kijani' itapimana misuli na
Ufaransa, huku timu ya taifa ya Algeria 'Mbweha wa Jangwani' itajitupa
uwanjani siku ya Jumanne kupambana na Ujerumani katika hatua ya 16
bora.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi karibuni Jiri Dvorak mjumbe
mwandamizi wa Kamati ya Afya ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA alisema
kuwa, wachezaji Waislamu watakaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani,
hawataathirika kiafya wakati wa kuendelea michuano hiyo nchini Brazil.
MUNIRA BLOG INAMUOMBA ALLAH AWAZIDISHIE IMAN NA IKHLASWI
0 comments:
Post a Comment