Jeshi
la polisi Zanzibar limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji ya
askari wa polisi na mgambo mmoja ambao waliuwawa kwenye tukio la
uvamizi wa kituo cha polisi cha Kimanzimchana walaya ya Mkuranga mkoa
wa Pwani Juni 11 mwaka huu.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa
huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa Kusini Pemba ACP Juma Yussuf Msige
amemtaja mtuhumiwa huyo kwa jina la Hamis Othman Mzee maarufu kwa jina
la Hamis Mabunduki na makachero walifanikiwa baada ya kufuatilia
nyendo zake na kumkamata wakati wa mchana akiwa mafichoni katika
kijiji cha Matale Chake Chake Pemba na hivi sasa wanawasilaina nawenzao
wa Pwani kwa ajili ya upelelezi zaidi
0 comments:
Post a Comment