BALOZI
wa zamani wa Vatican katika Jamhuri ya Dominica, Monsinyori Jozef
Wesolowski ametiwa hatiani na Mahakama ya Kanisa Katoliki kwa tuhuma za
kudhalilisha watoto.
Kutokana
na kutiwa hatiani huko amepokwa upadre wake. Monsinyori Wesolowski
amekuwa kiongozi wa juu kuteuliwa na Papa kutiwa hatiani na kupewa
adhabu hiyo ya kupokwa upadri.
Taarifa ya
Vatican ilisema Monsinyori Wesolowski alikutwa na hatia na Mahakama hiyo
ya Usharika wa Mafundisho ya Imani katika siku za hivi karibuni: kwa
adhabu hiyo ina maana hataweza kutekeleza majukumu yake kama Padre.
Wesolowski
amepewa miezi miwili ya kukata rufaa. Lakini pia anakabiliwa na
mashtaka katika Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Vatican. Kwa kuwa ni
Mwanadiplomasia wa Kipapa yeye ni raia wa mji wa nchi hiyo.
Papa
alimrejesha Vatican, Wesolowski ambaye ni mzaliwa wa Poland Agosti 21,
2013 na kumfuta kazi baada ya Askofu wa Santo Domingo, Kadinali Nicolas
de Jesus Lopez kumueleza Papa Francis kuhusu kuwepo kwa tetesi kuwa
Wesolowski aliwadhalilisha watoto wa kiume akiwa Jamhuri ya Dominica.
Mamlaka za Dominican hatimaye zilianza uchunguzi lakini hazikumshtaki. Poland, pia ilianza uchunguzi dhidi ya Wesolowski.
Wesolowski
ni Ofisa wa Juu Vatican kuchunguzwa kwa tuhuma za udhalilishaji watoto
na kesi yake iliibua waswali iwapo Vatican, kwa kumuondoka katika
mamlaka ya Dominica ilikuwa ni kumlinda na kuanzisha uchunguzi wake
kabla ya mamlaka za taifa hilo la Caribbean.
Hata
hivyo Vatican haijawahi kusema iwapo Wesolowski alishawahi kujitetea
kuhusiana na tuhuma hizo na hajawahi kutoa mawasiliano yoyote kwa
mawakili wake.
Kesi
hiyo imekuwa ikichukuliwa kwa umakini kwani Wesolowski alipewa
upadirisho wake na Uaskofu na Papa St John Paul 11 ambaye pia ni Raia wa
Poland.
0 comments:
Post a Comment