Feb 27, 2014

Njama ya kugawanywa nchi za Kiarabu yafichuka

Duru za habari kutoka Misri zimefichua mkakati uliopangwa na Marekani kwa kushirikiana na Qatar kwa lengo la kuzigawa vipande vipande nchi za Kiarabu. 

Gazeti la al Yaum as Saabi’i limeandika kuwa, Tamim bin Hamad wakati alipokuwa mrithi wa kiti cha Ufalme wa Qatar alikutana na kufanya mazungumzo ya siri na Seneta Lindsey Graham wa Marekani ambaye ni muungaji mkono mkubwa wa Israel tarehe 30 Mei 2011, na kufikia makubaliano ya kumuondoa madarakani Kanali Muammar Gaddafi wa Libya na kuigawa vipande vipande nchi ya Misri.
Mpango huo uliwahi kubuniwa na Marekani katika muongo wa 1980 ukijulikana kwa jina la Mashariki ya Kati Mpya, kwa lengo la kuzidhoofisha zaidi nchi za Kiarabu kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Kwa mujibu wa nyaraka hizo za siri, Qatar ilikubali kutoa kitita cha dola bilioni tatu hadi tano kwa lengo la kuigawa Misri.

0 comments:

Post a Comment