Shirika la Kutetea Haki za Binadamu
la Amnesty International limetangaza kuwa, majeshi ya utawala wa
Kizayuni wa Israel yanatenda jinai za kivita kwa kuwauwa na kuwajeruhi
wananchi wa Palestina walioko katika eneo la Ukingo wa Magharibi mwa Mto
Jordan.
Philip Luther, Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Kati na
Kaskazini mwa Afrika wa shirika hilo la kimataifa amesaema kuwa, kuna
ushahidi wa kutosha unaoonyesha kwamba majeshi ya Israel yametekeleza
mauaji dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Kipalestina katika eneo hilo.
Shirika la Amnesty International limeeleza kuwa, wanajeshi wa Israel
katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wamewauwa makumi ya wananchi
wa Palestina wasio na hatia.
Ripoti hiyo yenye kurasa 87 imeeleza kuwa,
wanajeshi wa Israel licha ya kutumia silaha za moto na nguvu kupita
kiasi, yamewauwa wananchi 45 wa Kipalestina na kuwajeruhi maelfu ya
wengine.
Shirika la Amnesty International limezitaka nchi za Marekani,
Umoja wa Ulaya, na wanachama wengine wa Jamii ya Kimataifa waache
kupeleka silaha na zana za kijeshi huko Israel, ili kuushinikiza utawala
huo uache kuwauwa Wapalestina.
0 comments:
Post a Comment