Mara baada ya serikali ya
Uganda na nchi nyingine duniani kupitisha sheria kali dhidi ya watu
wanaojihusisha na ngono za jinsia moja, Marekani imeanzisha mkakati mpya
wa kukabiliana na kile inachodai kuwa ni hatua dhidi ya haki za
binadamu.
John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani
ameifananisha kuwa ni dhidi ya Uyahudi na ubaguzi sheria kali iliyowekwa
na Uganda dhidi ya wanaolawitiana na wanasagana na kutaka serikali ya
Kampala iifute sheria hiyo haraka iwezekanavyo.
Kerry amesisitiza kuwa
ni makosa kuchukua hatua nyepesi za kidiplomasia dhidi ya sheria
zinazopiga marufuku vitendo vya liwati na usagaji barani Afrika.
Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani ameongeza kuwa, Washington
inakusudia kutoa amri kwa balozi zote za nchi hiyo ulimwenguni kuanza
kuchunguza changamoto zinazohusiana na kadhia hiyo.
Inafaa kuashiria
hapa kuwa, kuna nchi zisizopungua 80 duniani ambazo zimepiga marufuku
vitendo vichafu vya liwati na usagaji, na watu wanaopatikana na hatia
wanaadhibiwa adhabu ya vifungo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment