Imeelezwa kwamba Uislamu ndiyo Dini pekee isiyobadilishwa maandiko yako.
Hayo yamesemwa Jioni hii na Mhadhir wa kimataifa kutoka Uingreza Sheikh Adnan Rashid.
Akiwa hutubia Waislamu katika waliofika katika mhadhara huo,Sheikh Adnan (ambaye ameslimu) amesema Dini zote (isipokuwa Uislamu) maandiko yao ya awali (Vitabu vyao) vimebadilishwa.
"Ndugu zangu natoa ofa,kama yupo Mkristo au Myahudi ambaye amehifadhi japo ukurasa mmoja wa kitabu chake cha asili,basi aje hapa nimkabidhi mapaund (pesa za uingreza)"Alisema
Aidha alisema ni "Uislamu pekee ndiyo dini inayoweza kuleta amani katika diunia hii,zinaa,ukimwi,kuuana,kuroga,ulevi n.k hivi vyote vimekatazwa na uislamu,na pindi watu wakiviacha vitu hivi basi amani itatawala"
Aliongeza kwa kusema "katika kuonyesha uislamu umekamilika,mtume kaelekeza hata ukitaka kumchinja mnyama,basi umchinje sehemu ya faragha ili wenzake wasione,tena umnyweshe maji kabla ya kumchinja na uhakikishe kisu ni kikali,haya huyapati kwa dini isiyo ya uislamu"Mwisho wa kumnukuu.
Kwa mujibu wa Sheikh Adnan Uislamu unaeenea kwa kasi katika bara la Ulaya baada ya wengi kujuwa ukweli wa uislamu.
Mhadhara huo ulioandaliwa na taasisi ya AL MALID utaendelea tena kesho katika viwanja hivyo vya manzese mpakani,Jijini Dar es salaam.
SAA KUMI NA MOJA NA NUSU PADRI MR TONY LEONARD KUTOKA AUSTARIA AKIINGIA KATIKA VIWANJA VYA MANZESE MPAKANI KWA AJILI YA KUSHIRIKI KATIKA MHADHARA HUO.
PADRI MR TONY KUTOKA AUSTARIA AKISHIRIKI MHADHARA JIONI HII.
HAWA NI WAHADHIRI (MUSLIM) WA KIMATAIFA KUTOKA UINGREZA
0 comments:
Post a Comment