Jan 1, 2014

Nasrullah, shaksia wa mwaka 2013 nchini Lebanon

Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah ametajwa kuwa shakhsia wa mwaka 2013 huko Lebanon kufuatia uchunguzi wa maoni uliofanywa na shirika kuu la habari la nchini humo. 

Utafiti wa maoni ulioendeshwa na Shirika la Utangazaji la Lebanon unaonyesha kuwa Sayyid Hassan Nasrullah amepata zaidi ya asilimia 60 za kura.

Nasrullah aliye na umri wa miaka 53 amekuwa akiongoza harakati ya muqawama ya Hizbullah katika mapambano dhidi ya uchokozi na uvamizi wa Israel tangu mwaka 1992.

 Mwaka 1992 Israel ilimuua Abbas al Musawi, Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah, mkewe, mwanawe wa kiume na watu wengine wanne.  

Mwezi Juni mwakak 1982, wanajeshi wa Israel walilivamia eneo la kusini mwa Lebanon na kusalia huko hadi Mei mwaka 2000, ambapo baadae harakati ya Hizbullah iliwalazimisha wanajeshi hao maghasibu wa utawala wa Kizayuni kuondoka katika maeneo hayo.

0 comments:

Post a Comment