Dec 3, 2013

Waziri Mkuu Said Afukuzwa Kazi.

somalimemo.net 

Mohamed Uthmaan Jawaari Jana ametangaza kura zilizopigwa na Wabunge na kusema kuwa Utawala uliokuwa ukiongozwa na Waziri Mkuu wa Serikali Dhaifu ya Somalia TFG imeanguka baada ya malumbano ya Muda mrefu ambapo wabunge hao walikubaliano kwa asilimia nyingi kutokuwa na Imani nae Waziri Mkuu wa Serikali ya TFG.


Wanachama wa Bunge la TFG Jana kwa siku ya pili walikuwa na Kikao cha mfululizo mjini Mugadishu na hatimae kikao ulikamilika,Maofisa kutoka Kasri ya Rais waliokuwa na Pesa walikuwako kwenye Kikao hicho na kufanikiwa kuiangusha Serikali ya TFG baada ya kuwa ahidi wabunge hao Pesa.

Waziri Mkuu aliyefukuzwa kazi Said Shirdoon alipokuwa kwenye ofisi yake mjini Mugadishu alifanya mazungumzo na vyombo vya Habari na kudai kuwa ndani ya Serikali ya TFG kumeibuka Makundi Makundi kwa Maofisa wakuu wa Serikali na kuongeza kuwa ni Hatari uwepo kwa Serikali hiyo.

Spika wa Bunge alitangaza kuwa idadi ya wabunge 184 walipiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri mkuu wa Serikali ya TFG huko Wabunge wapato 65 walipiga kura ya kukubaliana na Waziri Mkuu na Wabunge wapatao 10 walinyamazia,Kelele na miruzi zilisikika ndani ya Holi ya Bunge hilo.

Hitilifu uliokuwapo katika siku za hivi karibuni umesababisha Wakuu wawili wa Serikali hiyo kila upande kumvutia na kumiliki wabunge wengi kwa kadri aliyetoa Dola nyingi za Kimarekani kama Rushwa kwa Wabunge hao.

0 comments:

Post a Comment