Zaidi ya watoto 1,000 hapa nchini huzaliwa na tatizo la vichwa vikubwa na uti wa mgongo kwa kila mwaka, ambapo kati yao watoto 250 tu ndiyo wanaofikishwa kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) kwa ajili ya matibabu.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Uhusiano wa Taasisi hiyo, Bwana Patrick Mvungi na kuongeza kama ninavyomnukuu: “Tatizo la ugonjwa wa kichwa kikubwa na uti wa mgongo ni kubwa na linazidi kuongezeka siku hadi siku.” Mwisho wa kunukuu.
Patrick amesema kuwa, katika kipindi cha awali cha ujauzito mama anatakiwa kutumia chakula chenye lishe bora na kwenda kliniki kwa wakati na kwamba, vinginevyo hupata upungufu wa madini ya Folic Acid.
Amesema kuwa watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo kwa mwaka ni zaidi ya 4,000 lakini watoto wanaopokelewa hospital kwa mwaka wanafikia 250 tu suala linalozidi kutia wasi wasi mkubwa.
Kwa upande mwingine ofisa uhusiano huyo amesema kuwa, watoto wanaozaliwa na wanaopokelewa hapo MOI ni tofauti kwa kuwa wengi wanaamini tatizo hilo linatokana na ushirikina hali inayowakosesha tiba na watoto wengine kupoteza maisha au kufichwa na wazazi wao.
0 comments:
Post a Comment