Jumamosi, Machi 29.

Dec 8, 2013

Wapalestina wapinga kufukuzwa Waarabu Naqba

Mamia ya wananchi wa Palestina wamendamana kupinga mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuwalazimisha makumi ya maelfu ya Wapalestina walioko katika jangwa la Naqba. 

Waandamanaji hao waliandamana katika miji ya Jaffa na Haifa ili kupinga mpango huo wa PRAVER, wa kuwafukuza Wapalestina 70,000 na kuharibu vijiji karibu 35 vya Wapalestina hao wanaoishi katika jangwa hilo. 

Mohammad Mahmid miongoni mwa waratibu wa maandamano hayo amesema, hatua hiyo ni maangamizi ya kizazi yanayofanywa na Wazayuni na kwamba lengo la kuwafukuza Wapalestina hao katika vijiji vyao na kuwakusanya mahala pengine ni kuhakikisha kwamba eneo la Naqba linakuwa la Wayahudi pekee.  

Maandamano kama hayo yalifanyika pia wiki iliyopita katika maeneo ya Haifa, Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza. Mpango wa kibaguzi wa Praver umebuniwa na Ehud Praver na Benny Begin viongozi wawili wa utawala wa Kizayuni na hivyo kujulikana kama mpango wa "Praver-Begin."

0 comments:

Post a Comment