Jumamosi, Aprili 5.

Dec 9, 2013

Waislaam zaidi ya 100 wateketezwa ndani ya Msikiti Afrika ya Kati.



Habari kutoka mjini Bangwi iliyo mji mkuu wa nchi ya Afrika ya Kati unaeleza kuwa mauaji ya mamia ya waislaam yamefanyika mjini hapo.

Msikiti mkuu wa Mji wa Bangwi jana ulikutwa miili ya waislaam wapatao zaidi ya 80 ambapo unaarifiwa waliuliwa usiku wa kuamkia tarehe 06,12,2013 ndani ya msikiti hiyo.


Duru zinaarifu kuwa Makundi ya Manswara waliokuwa na hasira walivamia mitaa ya Waislaam na hatimae waislaam walikimbilia msikitini kama eneo salama lakini Manaswara hawa kuwaacha bali waliingia hadi ndani ya msikiti na kufanya Mauaji hayo ya kinyama.

Mashirika ya Habari ziliarifu kuwa Waislaam na Wakristo mara kwa mara walikuwa wakipigana katika siku za Al-khamisi na Ijumaa na wakitumia Silaha za Kijadi kama Mapanga na Visu kwenye Barabara ya mji mkuu wa Nchi ya Afrika ya Kati.

Madaktari waliopo mji wa Bangwii wanaeleza kuwa Majeruhi wapatao 12 walichukuliwa kutoka Hospitalini na baadae kuuliwa kwa risasi na unahofiwa vita kuongezeka.

Muungano wa Wanamgambo wa Waasi wanaojulikana SILKA ambao wengi wa wanamgambo hao ni Waislaam na walipindua Rais aliyekuwako Madarakani Franso Bosisi mwezi March mwaka huu.

Vikosi vya Ufaransa waliofika mjini Bangwi Al-khamisi iliyopita wanasaidiana na kuwapa silaha wakristo na kuwashawishi kuwaua waislaam wa nchi hiyo.

Mji wa pili ambao ndio moja ya miji mikuu wa nchi ya Afrika ya Kati unashikiliwa na wanamgambo waasi wa Kislaam,japo si wanamgambo hao hawana fikra ya kuitawala kwa sheria za Kislaam kwenye maeneo wanaoishikilia.

Utawala wa France uliokuwa Koloni wa Nchi hiyo unajaribu kuhusika katika mauaji dhidi ya waislaam wa nchi ya Afrika ya Kati.

0 comments:

Post a Comment