Jun 7, 2013

DYCCC KUFANYA MITIHANI YA PAMOJA
KWA WANAFUNZI WA MADRASA.

Taasisi ya wayemen wanaoishi Dar es salaam (DYCCC) kupitia idara yake ya madrasa imeandaa mitihani ya pamoja kwa wanafunzi wa madrasa zilizo chini ya udhamini wao.

Hayo yalibainishwa na Sheikh Ramadhan Khamis Kwangaya ambae ni katibu mkuu wa idara ya madrasa ya dyccc.

Akiongea kwa njia ya simu na blog ya munira madrasa leo hii jioni,Sheikh Kwangaya amesema idara yake iliweka malengo makuu manne ambapo aliyataja kuwa ni pamoja na kuwapatia posho waalimu waliofaulu mitihani ya idara,kuwapatia mitaala,kuwapatia vitabu vya kiada pamoja na kufanya mitihani ya pamoja kwa wanafunzi wote wa madrasa zilizo chini ya udhamini wa idara hiyo.

"Tunamshukuru mungu kwa kuyafikia malengo yetu kwani tulianza kuwapatia posho kidogo waalimu wetu ili angalau wapate utulivu,baada ya hapo tuliwapa mafunzo ya namna ya kuitumia mitaala yetu kisha tukawapa vitabu vya kiada na sasa tunafanya mitihani ya pamoja" mwisho wa kumnuukuu.

Akijibu swali la mwandishi wa blog ya munira aliyetaka kujuwa kama walimu hao walipata muda wa kutosha wa kupata elimu na uzoefu,Sheikh kwangaya alisema,wanaimani tosha ya kwamba waalimu wao wameiva kimafunzo ya kutumia mitaala,kwani tokea mwaka 2006 wamekuwa wakiwapatia waalimu hao mafunzo hayo kwa njia ya semina na makongamano mbalimbali.
 

Sheikh kwangaya alisema hii ni awamu ya nne kufanya mitihani  hii ya pamoja tangu mwaka 2011 na kama idara wana matumaini makubwa ya kukuwa na kuboreka kwa ustawi wa elimu ya dini kwani itatoa taswira ya iwango vya elimu ya msingi katika madrasa (ibtadaiyyah).

Alisema licha ya jitihada na mafanikio kadhaa waliyoyapata lakini wanakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo alizitaja kuwa ni pamoja na gharama za mitihani zipo juu sana,hali ambayo ilimsukuma kuto wito  kwa jamii ya kiislamu kuiunga mkono idara hiyo kwa hali na mali.ili juhudi na ushindani uliopo hivi sasa baina ya wanafunzi kwa wanafuni na waaalimu kwa walimu zisije kutoweka.

mitihani hiyo itawashirikisha wanafunzi 850 wa madrasa thelathini na tatu zilizopo jijini Dar es salam,itafanyika tarehe 15/06/2013 shule ya DYCCC iliyopo Chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.

0 comments:

Post a Comment